WhatsApp Image 2022-10-03 at 9.32.39 AM

ROC SPORTS BONANZA

ROC YOUTH inakuletea tamasha zuri sana linaloitwa ROC SPORTS BONANZA⚽🏸
Ni siku ambayo vijana tunakutana pale kiwanja cha Hekima Garden – Mikocheni.
Tutakuwa na michezo mbalimbali…mpira wa miguu, mpira wa kikapu, dancing competition na surprises kibao ambazo tumekuandalia!
Unangoja nini??
Hakutokuwa na kiingilio kabisa, njoo tufurahi pamoja.
Tutakuwa na timu mbili..yaani TEAM PRAISE na TEAM MEDIA, chaguo ni lako ukae timu gani.Kuhudhuria utahitajika kujisajili kwa kututumia jina lako na Team uliyochagua… Mfano; “NAITWA ROSE JOHN – TEAM MEDIA” kisha tuma ujumbe wako kwenda number hii;
+255 654 477 060
Usipange kabisa kukosa!

@realityofchrist_
@rocmedia_
@rocworshipperz

WhatsApp Image 2022-09-28 at 6.38.22 AM

DODOMA DODOMA 🔥

DODOMA DODOMA 🔥

Kanisa la The Reality of Christ linapenda kukukaribisha sana mkazi wa Dodoma na miji jirani katika ibada ya Neno la Mungu na maombezi itakayofanyika leo kuanzia saa kumi na moja jioni pale ukumbi wa Dear Mama, Area C njia panda ya kuelekea Arusha.
Leo tutakuwa na muendelezo wa somo tuliloanza nalo wiki iliyopita linaloitwa TESO LENYE HAKI ikiwa ni sehemu ya pili.
Ibada itaongozwa na Mtumishi wa Mungu Disciple Godfrey Benjamin.
Karibu sana na Mungu akubariki.

@realityofchrist_
@sunbella_kyando
@minister_johnsembatwa
@siakyando
@rocmedia_

THE_YEAR_OF_UNLIMITED_SPEED

WhatsApp Image 2022-09-28 at 9.49.24 AM

Seminar – The END | Day 3

SEMINAR SEMINAR 🔥

Baada ya kujifunza kwa siku mbili mfululizo, leo tutakuwa na MAOMBEZI.
Ni wakati wa adui kuachilia kila baraka yako aliyoishikilia, ni wakati wa Mungu kuweka ukomo kwenye mateso maishani mwako!
Semina itaanza saa kumi na moja jioni hapahapa Reality of Christ, Sinza Mori karibu kabisa na ofisi za TAMWA na itaongozwa na Mtumishi wa Mungu Pastor John Sembatwa. Vilevile tutakuwa Live 🔴 kupitia ukurasa wetu wa YouTube wenye jina REALITY OF CHRIST CHURCH.
Karibu sana na Mungu akubariki.

@realityofchrist_
@sunbella_kyando
@minister_johnsembatwa
@siakyando
@rocmedia_

THE_YEAR_OF_UNLIMITED_SPEED

WhatsApp Image 2022-09-27 at 1.59.11 PM

MORNING GLORY 🔥

Mkazi wa DODOMA na miji jirani tunapenda kukukaribisha sana sana sana katika ibada hii itakayofanyika siku ya kesho(Jumatano) kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa moja kamili asubuhi, yaani MORNING GLORY.
Ibada itafanyikia palepale Ukumbi wa Dear Mama, Area C njia panda ya kuelekea Arusha na itaongozwa na Mtumishi wa Mungu Disciple Godfrey Benjamin.
Karibu sana na Mungu akubariki.

@realityofchrist_
@sunbella_kyando
@minister_johnsembatwa
@siakyando
@godfrey_thedisciple
@rocmedia_
#THE_YEAR_OF_UNLIMITED_SPEED

WhatsApp Image 2022-09-27 at 7.25.16 AM

Seminar – THE END

Baada ya jana kujifunza kuhusu chanzo cha mateso kwenye maisha ya mtu, leo tunaendelea mbele zaidi. Ni majira ambayo Mungu amekusudia aweke ukomo kwenye kila mateso kwenye maisha yako.
Semina itaanza saa kumi na moja jioni hapahapa Reality of Christ, Sinza Mori karibu kabisa na ofisi za TAMWA na itaongozwa na Mtumishi wa Mungu Pastor John Sembatwa. Vilevile tutakuwa Live 🔴 kabisa kupitia ukurasa wetu wa YouTube wenye jina REALITY OF CHRIST CHURCH ili hata wewe uliye mbali uweze kushiriki nasi baraka hii.
Karibu sana na Mungu akubariki.

@realityofchrist_
@sunbella_kyando
@minister_johnsembatwa
@siakyando
@rocmedia_
#THE_YEAR_OF_UNLIMITED_SPEED